Thursday, February 27, 2020

KARATA ZA SIASA TUM

Joto la  kisiasa linaendelea kukighubika chuo cha kiufundi cha Mombasa. Joto hili linawafanya wagombeaji tofauti kuwa na tumbo joto kutokana na hali ya kila mmoja wao kutokuwa na uhakika Wa kuibuka mshindi. Jamii mbalimbali nazo hazijawachwa nyuma. Kila jamii inafanya jitihada kuhakikisha kuwa itakuwa kati ya zile ambazo zitagawanya keki ya ushindi ifikapo tarehe kumi na nane mwezi Wa tatu.
Katika harakati za kuitengeneza mirengo tofauti ya kisiasa, jamii mbili zimeonekana kuwa na ubabe katika swala zima. Jamii hizi ni waluhya na wajaluo. Mrengo Wa Waluhya unaongozwa na Harry Sululu pamoja na Hailstrom Salasia. Upande mwingine, wajaluo wanaonekana kugawanyika katika mirengo miwili,mrengo  Wa kwanza ukimpigia upato Jacklinus Otiato na Wa pili ambao unaonekana kuwa na usemi zaidi ukimpigia upato George.
Tunalolisubiri ni utengenezaji Wa mirengo kamili ya kisisasa. Kufikia sasa, mrengo Wa Sululu almaarufu kama "Western Alliance" ama "Team kubwa' umeweza kuwaunganisha wagombeaji tofauti wakiwemo Harry Sululu, George, Birel Clara, Salasia na Koke kutoka Ukunda.
Tunalolisubiri ni kuona ni jamii zipi zitakuwa katika mrengo  upi  na ni zipi ambazo zitatemwa na mirengo ipi.
Hata hivyo, tuna kila sababu ya kujiuliza maswali mengi iwapo Yale yaliyotokea Jana ni uyabiri Wa Yale yanayokuja. Wasomi walioenda chuoni na kuwa na uwezo Wa kufikiria na akili badala ya kufikiria na mawe wanakikashifu kitendo cha vijana waliotumiwa na Jack Otiato kuuvuruga mkutano Wa wanajamii wenzake.
Hata hivyo, siasa ni kama mshumaa usiokuwa na mkesha. Letu ni jicho tu kuona ni nani ataamua kufikiria na mawe badala ya kufikiria na akili.!!

No comments:

Post a Comment